Monday, September 17, 2007

Du mshikaji bongo ni noma......

Hellow
guys am back home, jamani lazima niseme baada ya kurudi kutoka bondeni aambapo nilikaa kwa muda wa wiki mbili sasa ndo nakaribia kutua dia... tobaaa... vijinyumba hivyo? yallaaa kama nashuka porini au rubani kapotea.... au dharau ajisemee Joti wa ze Komedi mimi sijui but.... haya naland DIA, wenyewe tunauita eti " mwalimu nyerere internatinal airport is it?'' just i refer back to Jorberg, then To Port Elizaberth the small town compare to Dar wanao uwanja wa ndege mkubwa tena wa kisasa zaidi ya bongo. Hii si ni aibu kwa taifa hili lenye wasomi na watu zaidi ya milioni 35? Hivi nikuulize Mbongo mwenzangu hawa viongozi serikalini wanafanya nini? Kweli nilitamani nirudi SA nilivyokuwa napokelewa na vijumba- tena visivyo kwenye utaratibu maalum, hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania? nisemenini mie mwana wa Thonya mimi mkakati nilionao muda huu ni kusoma kwa bidii kwani nahisi bongo tunayeyushana.Kila kukicha viongozi wetu wanaenda nchi za nje hivi hata kuiga maendeleo ni shida au ndo mawazomgando.... Kudadadeki.
Ok nikizipata nitakuwa kama Ndesanjo nakaa zangu Ughaibuni nawachora tu wajukuu wa Mwalimu Nyerere.
Ni hayo tu kwa sasa

3 comments:

Ansbert Ngurumo said...

Nyie kina mama ndio mlimchagua mr handsome eti "Kikwete ana sura nzuri." Ebo! Kwani tunakwnda kuchumbia sisi? Mwalimu alishatuonya "kama ana sura nzuri mwalike mkanywe chai...si kumpa urais." Mmempa, sasa du! Yumo kwenye kikso cha maangamizi. Soma Maswali Magumu, Tanzania Daima Jumapili Septemba 23, 2007.

Anonymous said...

Dadangu, Nchi yoyote ile ulimwenguni hujengwa na wazalendo wa nchi husika. Ulichokiona south africa hakikushuka kutoka mbinguni, bali watu walifanya kazi kwa bidii yote na hayo ndo matokeo yake. Tusifikiri kuzikimbia nchi zetu kwa sababu ya umaskini wake, bali tujenge mikakati mbadala wa kuondokana na hii hali inayotuchefua. Kurudi nyuma hakuna maana nikizingatia ya kwamba si wote watakaohama na wewe nikimaanisha baba, mama, dada, kaka, mjomba na shangazi wote hawa wanakuangalia kutokana na ujamaa wetu wa extended families. Cha msingi ni kuanza kuweka kwenye vitendo kile unachofikiri kiliifanya afrika ya kusini kufikia hapo ilipo. Asante.

Anonymous said...

uslaumu jenga nyumba yako ya nguvu tuione usione vyaelea vimeundwa